Jumamosi, 23 Machi 2019

UAMINIFU

_*• Jamaa mmoja alienda kukata miti porini.. wakati anakata ghafla Panga lake likadondoka mtoni...akaanza kulalamika sana...*_

_*• Malaika akatokea na kumuuliza kwanini analia..*_

_*• Jamaa akamjibu nimedondosha panga langu mtoni na ndiyo natumia kuendesha maisha yangu..*_

_*• Malaika akazama mtoni akatoa panga la Dhahabu akamuuliza ndiyo hili??*_

_*• Akajibu Hapana...*_

_*• Malaika akazama tena akatoa panga la shaba, akamuuliza ndiyo hili??*_

_*• Jamaa akajibu HAPANA.*_

_*• Malaika akazama tena akaibuka na panga la bati, akamuuliza ndiyo hili..*_

_*• Jamaa akajibu NDIYO..*_

_*• Malaika akapenda uaminifu wake na kumpa mapanga yote matatu aende nayo..*_

_*• JAMAA akafurahi sana..*_

_*• Siku nyingine Jamaa alikuwa anatembea na mke wake njiani, ghafla Mke wake akadondoka mtoni. jamaa akaanza kulia.....*_

_*• Malaika akatokea tena na kumuuliza mbona unalia.*_

_*• Jamaa akamjibu, mke wangu kadondoka mtoni..*_

_*• Malaika akazama mtoni akaibuka na MASOGANGE.. Akamuuliza huyu ndiyo huyu.*_

_*• Jamaa akajibu, NDIYO..*_

_*• Malaika akakasirika na kumwambia Kwanini umenidanganya..*_

_*• Jamaa akamjibu..nimesema ndiyo sababu najua ningesema HAPANA Ungezama ungemtoa AUNTI EZEKIEL ... ningesema HAPANA ungezama na kumtoa mke wangu alafu ningesema NDIYO ungenipa wote Watatu niondoke nao...... Sasa mimi ni Masikini sina uwezo wa kuhudumia wote hao.... ndiyo maana nikasema ndiyo Kwa Masogange.*_

*• SOMO LA KUJIFUNZA..*
_*• Wanaume huwa hatusemi uongo bila sababu....

YouTube. CC3 
Whatsapp. 0757215974
Instagram. Barakamanyota 
Fb. Baraka manyota 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

share

Chapisho Lililoangaziwa

MTAZAMO

Tafiti zinaonyesha kuwa watu ambao shuleni walikuwa wanapata ziro wakiwa mtaani huwa wana uwezo mkubwa sana wa kuzijua njia za kutafuta pesa...